IQNA

Usomaji wa Qur’an wa mwana wa afisa wa Hamas aliyeuawa shahidi (+Video)

21:58 - September 16, 2025
Habari ID: 3481244
IQNA – Video ya Tarteel ya Qur’an iliyosomwa na shahidi Hammam al-Hayya, mwana wa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Khalil al-Hayya, ambaye aliuawa shahidi hivi karibuni nchini Qatar, imesambazwa mtandaoni.

Hammam, pamoja na wenzake wanne akiwemo askari wa usalama wa Qatar, waliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la Israeli lililolenga mkutano wa maafisa wa Hamas mjini Doha wiki iliyopita.

Klipu inayofuata inaonesha usomaji wa Shahidi Hammam wa Qur’an kwa Tarteel katika mazishi ya watoto na wajukuu wa shahidi Ismail Haniyeh, aliyekuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, ambaye aliuawa shahidi na Wazayuni nchini Iran Julai mwaka jana.

Hammam alisoma aya 154 hadi 157 za Surah al-Baqarah zinazohusu mashahidi, mbele ya babake na wageni wa heshima waliohudhuria hafla hiyo.

Tarehe 9 Septemba, utawala wa Kizayuni ulifanya mashambulizi ya angani dhidi ya makao makuu ya Hamas mjini Doha, katika kile kilichoelezwa kama “operesheni ya mauaji ya kulenga,” ambapo wanachama kadhaa wa harakati hiyo na afisa wa usalama wa Qatar waliuawa.

Viongozi wa juu wa Hamas akiwemo Khalil al-Hayya, Khaled Meshal, na Zaher Jabarin waliokoka jaribio hilo la mauaji.

Baada ya shambulio hilo la kinyama, Qatar ililaani mashambulizi ya Israeli ikiyataja kama “ugaidi wa kiserikali,” na ikaahidi kujibu ipasavyo.

4304958

captcha