IQNA

Ujumbe wa Al-Azhar kuhudhuria mkutano wa vongozi wa dini duniani nchini Kazakhstan

21:49 - September 16, 2025
Habari ID: 3481243
IQNA – Ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri utashiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Viongozi wa Dini za Dunia na Jadi utakaofanyika Kazakhstan.

Mkutano huo utaanza Jumatano, Septemba 17, kwa kuhudhuriwa na Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev, katika mji mkuu Astana.

Kituo cha Mazungumzo ya Kidini cha Astana ndicho kitakachokuwa mwenyeji wa kikao hiki cha siku mbili.

Sheikh Ahmad al-Tayyib, Mkuu wa Al-Azhar na Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu, amemteua Naibu wake, Profesa Mohammad al-Duwaini, kuongoza ujumbe wa Al-Azhar katika kongamano hili.

Ushiriki wa Al-Azhar katika mkutano wa Astana umetokana na mwaliko rasmi wa Rais wa Kazakhstan kwa Sheikh Mkuu wa Al-Azhar.

Katika toleo lililopita mwaka 2022, mkutano huu uliweka historia kwa kuhudhuriwa na Sheikh al-Tayyib pamoja na Baba Mtakatifu Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki wakati huo.

Mkutano wa Viongozi wa Dini Duniani na Jadi ni tukio la kimataifa linalofanyika mara kwa mara mjini Astana, kwa lengo la kukuza mazungumzo kati ya viongozi wa dini ili kukabiliana na changamoto za kijamii, kitamaduni na kidini.

Wawakilishi wa dini mbalimbali hushiriki katika mkutano huu, ambao mbali na mijadala rasmi, hujumuisha pia matukio ya kimaashirio yanayodhihirisha thamani za amani na kuishi kwa pamoja.

3494609/

Habari zinazohusiana
Kishikizo: kazakhstan al azhar dini
captcha