Mkutano wa kwanza, uitwao Qurani Tukufu na Maarifa ya Kibinadamu: Kuelekea Uelewa Ulio Komaa wa Mwanadamu, utawakutanisha zaidi ya watafiti 18 kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Qatar, mkutano huo utajadili namna Qur'ani inavyoweza kuchangia katika kuunda maarifa ya kijamii na kibinadamu, kwa kuangazia nyanja za elimu, jamii, saikolojia, na uchumi.
Waandaaji wamesema lengo ni kuhimiza mazungumzo baina ya wanazuoni wa fani za dini na wale wa sayansi za kijamii na kibinadamu. Aidha, mkutano huo utatafuta njia za kuunganisha tafsiri za Qur'ani na mbinu za kisasa za utafiti, na kutumia matokeo hayo kuchunguza masuala ya kijamii.
Mkutano wa pili, uitwao Jukwaa la Kitabu cha Kwanza cha Ummah, utapitia mfululizo wa Kitabu cha Ummah ambao umeendeshwa kwa zaidi ya miaka arobaini. Mfululizo huo umechunguza masuala ya kiutamaduni na kiakili ndani ya ulimwengu wa Kiislamu.
Jukwaa hili litajadili mbinu na mitazamo ya mfululizo huo, sambamba na umuhimu wake katika masuala ya sasa. Karatasi nane za kazi zitawasilishwa, zikilenga jinsi maadili ya Kiislamu yanavyoweza kuchangia katika kufufua utamaduni na kusaidia kujenga utambulisho wa Muislamu ulio na mizani katika mazingira ya dunia yanayobadilika kwa kasi.
3494777