Kwa mujibu wa taarifa ya IQNA kupitia Televisheni al-Masirah, Abdul Malik al-Houthi, kiongozi wa Ansarallah ya Yemen, katika hotuba aliyotoa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashem Safiyyuddin , alisema: "Tunatoa pole tena kwa umma wa Kiislamu na ndugu zetu katika Hizbullah na harakati ya upinzani ya Lebanon na taifa la Lebanon. Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, Allah amrehemu, yuko katika akili ya watu huru duniani, na mwelekeo wake katika jihadi na upinzani unaendelea."
Abdulmalik al-Houthi amesemam kuwa kiongozi wa muqawama wa Lebanon shahidi Sayyid Hassan Nasrallah bado ni jinamizi kwa Israel ingawa aliuawa na utawala huo mwaka mmoja uliopita.
Abdulmalik ameongeza kusema: Baada ya Hizbullah kuibuka na ushindi dhidi ya Israel katika vita vya mwaka 2006, mradi uliokuwa umebuniwa na Marekani wa "Mashariki ya Kati Mpya" wa kubadili mazingira ya kijiipolitiki ya Mashariki ya Kati ulisambaratishwa na mashujaa wa Lebanon.
Aliongeza: Hizbullah sio peke yake na haitakuwa peke yake. Chama hiki ni sehemu ya mhimili, sehemu ya umma wake na pia ni kiongozi katika medani hizi za kukabiliana na mpango hatari zaidi wa uvamizi unaolenga umma wote, na umma wetu wa Kiislamu uko mstari wa mbele katika hilo. Ukweli, pamoja na matukio na mabadiliko yake yote na ukatili wa Israeli ambao umejulikana kwa ulimwengu wote, unathibitisha usahihi wa chaguo la jihadi na upinzani. Chaguo la jihadi na upinzani ni la lazima na hekima kwa sababu hakuna mbadala wa hiyo isipokuwa chaguo la kukubali. Umma wa Kiislamu na jamii ya kibinadamu mbele ya mpango wa Kizayuni, lazima ichukue hatua au ikubali."
Amesema Sayyid Hassan Nasrullah alisaidia kusitisha njama zilizokuwa zikiongozwa na Wazayuni za kueneza kushindwa miongoni mwa mataifa ya Kiislamu.
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa Sayyid Hassan Nasrullah alisimama kama mlimamrefu dhidi ya mradi Mpya wa Mashariki ya Kati uiotangazwa na Marekani wakati huo.
Ameongeza kuwa: Hizbullah haiko peke yake na haitakuwa peke yake. Chama hiki ni sehemu ya mhimili, sehemu ya umma wake na pia ni kiongozi katika medani hizi za kukabiliana na mpango hatari zaidi wa uvamizi unaolenga umma wote, na umma wetu wa Kiislamu uko mstari wa mbele katika hilo. Ukweli, pamoja na matukio na mabadiliko yake yote na ukatili wa Israeli ambao umejulikana kwa ulimwengu wote, unathibitisha usahihi wa chaguo la jihadi na upinzani. Chaguo la jihadi na upinzani ni la lazima na hekima kwa sababu hakuna mbadala wa hiyo isipokuwa chaguo la kukubali. Umma wa Kiislamu na jamii ya kibinadamu mbele ya mpango wa Kizayuni, lazima ichukue hatua au ikubali."
4307408