Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Sayyid Mahmoud Chavoshi, vyeti hivyo vilitolewa kupitia ofisi kuu baada ya programu za kina za elimu zilizoendeshwa na matawi na vituo vya taasisi hiyo kote nchini, zikilenga kuhifadhi na kufahamu Qur'ani.
Amesema, “Vyeti vilitolewa kwa kuhifadhi Juzu moja, tatu, saba, kumi na tano, ishirini, na ishirini na tano za Qur'ani.” Aidha, vyeti vilihusisha kukamilisha masomo 24, 48, na 72 kutoka katika vitabu vya mtaala wa taasisi vinavyoangazia maana na dhana za Qur'ani.
Waliopewa vyeti walitoka katika matawi ya taasisi yaliyopo katika mikoa 14 ikiwemo Tehran, Isfahan, Khorasan Razavi, Mazandaran, na Yazd.
Chavoshi aliongeza kuwa wale waliokamilisha kuhifadhi Juzu kumi na tano walipewa nakala ya juzuu tano za tafsiri teule ya Qur'ani, huku waliokamilisha Juzu ishirini na tano wakastahiki kushiriki mtihani wa kitaifa wa Sauti ya Wahyi, mtihani wa kuhifadhi Qur'ani yote unaojumuisha tafsiri na maana.
Taasisi ya Mahd Qur'an ilianzishwa mwaka 1992 kama shirika lisilo la kibiashara, likiwa na lengo la kufundisha Qur'ani, kuandaa walimu, na kulea wahifadhi wa Qur'ani Tukufu.
3494788