IQNA

Msomi wa Kiiraqi asisitiza umuhimu wa Umoja wa Kiislamu kama dhamira ya dharura

20:48 - September 17, 2025
Habari ID: 3481245
IQNA – Mwenyekiti wa Baraza la Wasomi wa Rabat Muhammadi nchini Iraq amesema kuwa umoja wa Kiislamu sasa ni jambo la lazima kutokana na changamoto nzito zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu.

Seyyed Abdulqader Al-Alousi alitoa kauli hiyo katika mahojiano na IQNA pembeni ya Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu uliofanyika Tehran wiki iliyopita, sambamba na maadhimisho ya miaka 1,500 tangu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

“Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume au Milad un Nabii ni njia yenyewe ya kuelekea kwenye umoja wa Kiislamu, na hili ni jambo ambalo Waislamu wote wanakubaliana nalo,” alisema Al-Alousi.

Alibainisha kuwa ummah wa Kiislamu uliibuka kwa baraka ya kuzaliwa kwa Mtume (SAW), na umeendelea na safari yake tangu hapo. “Leo, katika maadhimisho ya miaka 1,500 ya kuzaliwa kwa Mtume, tunaona kuwa ummah unapaswa kulitumia tukio hili kama fursa ya kuungana kwa neno moja,” aliongeza.

Msomi huyo alionya kuwa Waislamu wanakabiliwa na “hatari kubwa,” huku maadui wakipanga njama dhidi yao kutoka kila upande.

Alisisitiza kuwa masaibu ya Gaza na Palestina hasa yanahitaji mshikamano wa Waislamu. “Umoja wa Kiislamu, kwa kuzingatia hali hatarishi ya ummah, umekuwa hitaji la dharura,” alisema Al-Alousi.

Alipoulizwa jinsi Waislamu wanavyoweza kuiga mfano wa Mtume katika maisha ya kila siku, alielezea sunna ya Mtume (SAW) kama “mfano wa kujenga utu wa mwanadamu.”

Mtume Muhammad (SAW) alisema, alitumwa “kurejesha ubinadamu katika asili yake halisi.” Al-Alousi aliwahimiza Waislamu kuyafanya maisha ya Mtume (SAW) au Sira yake kuwa marejeo na kumwasilisha kwa ulimwengu kama “kielelezo cha ukamilifu wa kibinadamu.”

3494637

captcha