IQNA

Ombi la kupigwa marufuku ujasusi kwenye misikiti ya Marekani

12:14 - September 04, 2011
Habari ID: 2180910
Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani limeitaka halmashauri ya New York na Meya wa mji huo Michael Rubens Bloomberg, kupiga marufuku ujasusi katika misikiti na vituo vya Waislamu na vilevile kuzuia vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya jamii za wachache katika mji huo.
Ombi hilo limetolewa baada ya kufichuliwa ushirikiano mkubwa uliopo baina ya polisi ya New York na shirika la ujasusi la Marekani CIA dhidi ya Waislamu wa mji huo.
Ufichuaji huo ambao ulifanywa na shirika la habari la Associated Press unabaini kwamba majasusi wa shirika hilo kwa ushirikiano wa polisi wa upepelezi wa Marekani FBI, wamekuwa wakiingia kwa siri katika vituo vya jamii za Waislamu kwa madhumuni ya kufuatilia kwa siri shughuli na mienendo yao na hata kusikiliza mazungumzo yao ya simu na kisha kukusanya ripoti zinazopatika na kuzituma kwenye makao makuu ya CIA ili zitumike dhidi ya Waislamu.
Waislamu wanasema kuwa ujasusi unaofanywa dhidi yao na vyombo vya usalama vya Marekani unakwenda kinyume na Katiba ya nchi hiyo inayozuia kufanyika ujasusi dhidi ya raia wa nchi hiyo. 853775
captcha