Mafunzo hayo yatasimamiwa na Jumuiya ya Ustawi na Utafiti wa Kiislamu ya London katika siku za tarehe 10, 11, 17 na 18 Disemba.
Vikao vya mafunzo hayo vitachunguza maisha, mafundisho na turathi ya Nabii Muhammad SAW kwa mujibu wa aya za Qur'ani Tukufu.
Baadhi ya mada zitakazojadliwa katika masomo hayo ni pamoja na mafunzo ya kuitambua nafsi kutoka kenye sira ya Mtume, maisha ya miaka 63 ya mtukufu huyo, maisha ya Nabii Muhammad SAW katika mtazamo wa Qur'ani, Nabii Muhammad kama mwalimu, baba, mume na kiongozi na mafundisho ya Mtume Muhammad katika karne ya 21.
Mafunzo hayo yatatolewa na Sheikh Hassan al Banna, mkurugenzi na mwasisi wa Jumuiya ya Ustawi na Utafiti wa Kiislamu (IIDR).
Washiriki katika mafunzo hayo watapata elimu ya maneno 1000 yaliyotumiwa katika Qur'ani Tukufu, visa, ujumbe na darsa za Qur'ani. Vilevile wataelimishwa kuhusu somo la Qur'ani juu ya maendeleo ya mtu binafsi na jinsi ya kutekeleza mafundisho ya Qur'ani katika maisha ya kila siku. 854895