Kwa mujibu wa gazeti la al-Ahram linalochapishwa Misri, filamu hiyo itatengenezwa na Yahya al-Fakhrani, msanii mashuhuri wa Misri ambaye huko nyuma pia alitengeneza filamu nyingine ya visa vya wanyama katika Qur'ani.
Baadhi ya visa ambavyo tayari vimechaguliwa kwa jili ya kutengeneza filamu hiyo ni pamoja na As'habul Ukhdud, Nabii Musa na Hadhrat Khidhr (as), Talut na Jalut, Watu wa Peponi, Hakimu Luqman, Qarun na Dhul Qarnein.
Al-Fakhrani amesema kuwa amechukua uamuzi wa kutengeneza filamu hiyo baada ya kupokelewa vyema filamu yake ya kwanza iliyohusiana na visa vya wanyama kwenye Qur'ani Tukufu ambayo ilionyeshwa katika kipindi cha mwezi mtukufu uliopita wa Ramadhini.
Mwandishi wa filamu hiyo Ahmad Bahjat amesema kuwa tayari sehemu 15 za filamu hiyo zimewekwa tayari kwa ajili ya upigaji picha. 890459