IQNA

Ubelgiji yawawekea vikwazo Waislamu katika uchinjaji wa wanyama

20:03 - November 06, 2011
Habari ID: 2218545
Serikali kuu ya Ubelgiji imepitishia sheria isiyo ya Kiislamu inayowalazimisha Waislamu wote wa nchi hiyo kufisha ganzi wanyama wao kabla ya kuwachinja katika siku ya Idul Adh'ha.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Wafd linalochapishwa Misri, Waislamu wa Ubelgiji na hasa wanaoishi katika mji wa Antwerp, ambao kama walivyo Waislamu wengine katika siku hizi tukufu, wanajishughulisha na shamrashamra za kusherehekea Skuikuu ya Idul Adh'ha kwa kuchinja wanyama, wataruhusiwa tu kuchinja wanyama wao baada ya kuwafisha ganzi, jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya Kiislamu.
Serikali ya Ubelgiji imechukua hatua hiyo baada ya kuombwa kufanya hivyo na Jumuiya eti ya Kutetea Wanyama na kupitisha sheria hiyo masaa machache kabla ya kusherehekewa Idul Adh'ha nchini humo.
Jambo hilo limewakasirisha sana Waislamu kwa kutilia maanani kwamba kufishwa ganzi wanyama kabla ya kuchinjwa ni jambo linalopingana na misingi ya Kiislamu.
Katika kutoa radiamali yao kuhusiana na sheria hiyo, Waislamu wa Ubelgiji wamekuwa wakichapisha matangazo ya kuonyesha njia sahihi za uchinjaji wanyama katika Uislamu na kuyabandika ukutani katika misikiti na nyumba zao.
Waislamu pia wametaka kukutana na viongozi wa Baraza la Mji wa Antwerp na kuwafahamisha mafundisho ya Kiislamu yanavyosema kuhusiana na suala la uchinjaji wanyama.
Jumuiya ya Kutetea Wanyama ya Ubelgiji imeweka mitambo ya kufisha ganzi wanyama katika vichinjio vya nchi hiyo ili kuwalazimisha Waislamu watii amri hiyo ya kidhulma kabla ya kuwachinja wanyama kwa ajili ya Sikukuu ya Adh'ha. 894044
captcha