IQNA

Indipendent:

Kutiwa mbaroni Saiful Islam ni tishio kwa viongozi wa nchi za Magharibi

16:34 - November 21, 2011
Habari ID: 2226357
Kutiwa mbaroni mwana wa dikteta wa zamani wa Libya Saiful Islam Gaddafi ni tishio na hatari kubwa kwa viongozi wa nchi za Magharibi kwa kutilia maanani kuwa ana siri nyingi kuhusu uhusiano wa baba yake na shakhsia wengi wa kisiasa wa Magharibi.
Hayo yameandikwa na gazeti la The Independent la Uingereza katika toleo lake la jana. Limeongeza kuwa Saiful Islam Gaddafi ana habari nyingi za uhusiano wa baba yake na nchi za Magharibi na kukamatwa kwake kutafichua siri nyingi za uhusiano wa utawala uliopinduliwa wa Libya na Wamagharibi, suala ambalo ni tishio kwa viongozi wa nchi za Magharibi.
Independent limeandika kuwa iwapo Saiful Islam hatauawa au kuteswa na kunyanyaswa, yumkini akafichua uhusiano wa siri wa baba yake na marais wa nchi za Magharibi hususan makubaliano ya siri kati ya Gaddafi na viongozi wengi wa nchi za Magharibi.
Ripoti ya Independent imeandika kuwa miongoni mwa watu ambao kuna uwezekano faili lao likafichuliwa na Saiful Islam ni Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair na shakhsia wengine kadhaa mashuhjuri ambao walikuwa na uhusiano mkubwa na Gaddafi na Saiful Islam mwenyewe.
Saiful Islam Gaddafi alitiwa nguvuni Jumamosi iliyopita na wanamapinduzi wa Libya katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo na kusafirishwa kwa helikopta hadi kwenye mji wa Zintan ulioko kaskazini mwa nchi hiyo. 902277

captcha