IQNA

Saudia yalaaniwa kwa kuvunjia heshima misikiti ya Bahrain

12:30 - November 30, 2011
Habari ID: 2231862
Jumuiya ya Kiislamu ya Wifaq Milli ya Bahrain imetoa taarifa ikilaani vikali hatua mpya ya utawala wa Saudi Arabia ya kubadilisha msikiti mmoja uliouharibu hivi karibuni nchini Bahrain na kuufanya kuwa bustani ya umma.
Jumuiya hiyo imesema kuwa imesikitishwa mno na hatua ya utawala wa Saudia ya kuubadilisha msikiti ulioharibiwa wa Abu Dhar katika mtaa wa an-Nuweidarat nchini Bahrain na kuufanya kuwa bustani ya umma. Taarifa hiyo imesema hatua hiyo ni dharau na uvunjiwaji heshima wa wazi thamani za Kiislamu na hisia za wananchi wa Bahrain.
Jumuiya ya Wifaq imesema kuwa hoja zilizotolewa na utawala wa Saudi Arabia kuhusiana na sababu za kuharibiwa msikiti huo na mwingine katika eneo la Barbura zinagongana na kwamba matokeo ya uchunguzi uliofanywa na kamati ya kutafuta ukweli kuhusiana na suala hilo inabaini wazi kwamba sababu zilizopelekea kubomolewa misikiti hiyo ni za kiusalama na wala sio kama wanavyodai maafisa wa Saudia na wa Bahrain kwamba misikiti hiyo haikuwa na vibali vya ujenzi. 908313
captcha