Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto UNICEF, mwaka jana utawala huo ghasibu uliua watoto tisa wa Kipalestina na kuwajeruhi wengine 308.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa utawala haramu wa Israel unawashikilia mateka watoto 164 wa Kipalestina walio kati ya umri wa miaka 12-17.
Ripoti hiyo inadokeza kuwa watoto 20 wa Kipalestina waliteswa wakiwa katika korokoro za Israel na hata Wazayuni walijaribu kuwatumia watoto hao kama majasusi lakini walikataa.
UNICEF imeongeza kuwa utawala haramu wa Israel umekataa kutoa huduma za matibabu kwa watoto 27 wagonjwa katika ukanda wa Ghaza. AIdha ripoti hiyo imesema watoto 78 walipoteza makao yao katika kipindi cha miezi miwili iliyopita baada ya utawala wa Kizayuni kuharibu nyumba za familia zao katika Ukingo wa Magharibi.
918633