Kapteni Mehdi Meydani amemwabia mwandishi wa IQNA kuwa hayo yatakuwa ni mashindano ya 4 kati ya majeshi ya nchi hizi mbili jirani za Kiislamu.
Ameongeza kuwa Oman itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo yatakayofanyika mwezi Februari. 'Mashindano hayo yatakuwa na vitengo vya kuhifadhi juzuu 5, 10, 20 na Qur'ani nzima, amesema na kuongeza kuwa majeshi ya nchi mbili yatakuwa na washiriki watatu katika kila kitengo.
Kapteni Meydani amesema kuwa wawakilishi wa Iran ambao watatoka katika Jeshi la Taifa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, Jeshi la Polisi na Wizara ya Ulinzi watatangazwa hivi karibuni.
Mkuu huyo wa Darul Qur'ani katika jeshi la Iran amesema mashindano ya kirafiki ya Qur'ani kati ya majeshi ya Iran na Oman yalifanyika kwa mara ya kwanza nchini Iran.
927361