IQNA

Kikao cha Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu kufanyika Tunisia

19:01 - January 12, 2012
Habari ID: 2255862
Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Kiislamu wa Kifedha utafanyika Juni 22-23 mwaka huu wa 2012 mjini Sfax nchini Tunisia.
Kitivo cha Uchumi na Menejmenti cha Chuo Kikuu cha Sfax kimeandaa kongamano hilo chini ya anwani ya ‘Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu na Ustawi: Zakat, Sukuk, Talaful, Biashara , Umasikini, Uadilifu na Asasi Ndogondogo za Fedha’.
Katika hali ambayo misingi ya mfumo wa Kifedha wa Kiislamu iko katika Qur’ani na Sunna, bado Waislamu hawajafaidika kikamilifu na mfumo huu unaozingatia maadili.
Mkutano huo utawaleta pamoja wasomi, wataalamu na wafanyakazi katika sekta ya kifedha ya Kiislamu. Hii itakuwa ni mara ya kwanza mkutano huo kufanyika mjini Sfaz na ni fursa nzuri ya kutafakari kuhusu fursa za mfumo wa kifedha wa Kiislamu kwa ajili ya maendeleo ya kieneo na kupambana na umasikini pamoja na ubaguzi wa kijamii.
Aidha kikao hicho kinatarajiwa kutoa fursa kwa watafiti vijana kuwasilisha kazi zao katika sekta mbalimbali za mfumo wa kifedha wa Kiislamu.
933488
captcha