Wakiwa katika ukingo wa Mto Tongi karibu na mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka, Waislamu takribani milioni 4 wamehutubiwa na wanazuoni mbalimbali. Ijtimai hiyo ilidumu kwa muda wa siku tatu ambapo washiriki walisimamisha sala, kusoma Qur’ani na kusikiliza hotuba za wanazuoni kuhusu mafundisho ya Kiislamu.
Ijtimai hii ilianza mwaka 1966 na tokea wakati huo hufanyika kila mwaka nchini Bangladesha. Ijtimai hii hufanyika kwa himaya ya Harakati ya Kiislamu ya Tabligh Jamaat. Hotuba katika Ijtimai hiyo zilitolewa kwa lugha za Kiarabu, Kibangali, Kiingereza, Kiurdu na lugha zinginezo duniani.
Kati ya viongozi wa Bangladesh waliohudhuria Ijtimai hiyo ni Rais Zillur Rahman, Waziri Mkuu Sheikha Hasina, Kiongozi wa Upinzani Khaleda Zia, mawaziri na viongozi wa kisiasa.
Bangladesh ni nchi ya Kiislamu yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 144 .
936047