IQNA

Kongamano la Kimataifa la Amir Abdulqadr al-Jazairi kufanyika karibuni

13:07 - February 20, 2012
Habari ID: 2277428
Kongamano la Kimataifa la Amir Abdulqadr al-Jazairi kiongozi wa Harakati ya Kiislamu limepangwa kufanyika katika mji wa Tlemcen nchini Algeria tokea tarehe 25 hadi 29 mwezi huu wa Februari.
Kwa mujibu wa tovuti ya liberte-algerie kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Historia ya Algeria katika fremu ya ratiba za kuadhimishwa mji wa Tlemcen kama mji mkuu wa utamaduni wa Kiislamu katika mwaka 2012 ambapo mamia ya watafiti, wanafikra, wasomi, wataalamu wa masuala ya falsafa ya Kiislamu, wanahistoria na wahadhiri wa vyuo vikuu vya ulimwengu wa Kiislamui wanatazamiwa kushiriki.
Mapambano ya Waislamu wa Algeria yanatathminiwa katika mitazamo miwili tofauti. Wa kwanza ni kuwa Waislamu wa nchi hiyo walianzisha mapambano kwa ajili ya kuwafukuza wakoloni nchini kwao na wa pili ni kuwa waliamua kuanzisha mapambano na kuhuisha harakati za kisiasa za Kiislamu nchini kwa madhumuni ya kurejesha utukufui wa Kiislamu, baada ya utawala wa nchi hiyo kupuuza masuala na mafundisho ya Kiislamu.
Ili kupambana na ukoloni wa kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi wa Ufaransa, wananchi wa Algeria walifanya harakati nyingi za mapambano dhidi ya wakoloni hao ambapo mapambano ya miaka minane yaliyoongozwa na Amir Abdulqadr al-Jazairi mwanzoni mwa ukoloni huo ndiyo mapambano yanayojulikana zaidi nchini humo.
Mapambano yaliyofanyika nchini Algeria kabla ya uhuru wa nchi hiyo kimsingi yaliongozwa na wanazuoni wa Kiislamu. Amir Abdulqadr alikuwa mwanazuoni wa kwanza kuongoza mapambano hayo ya harakati ya Kiislamu dhidi ya wakoloni wa Ufaransa. 956644
captcha