IQNA

Ahmadinejad asema Wamagharibi wameshindwa kuunusuru utawala wa Kizayuni

14:47 - February 27, 2012
Habari ID: 2281607
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa juhudi za madola ya kibeberu duniani za kuunusuru utawala wa Kizayuni usiangamie zimegonga mwamba.
Rais Ahmadinejad amesema kuwa madola ya kibeberu duniani yanazishinikiza harakati za ukombozi ili kuunusuru utawala wa Kizayuni ulio dhidi ya binadamu, hata hivyo hapana shaka kwamba lengo hilo halitafanikiwa. Rais wa Iran ameyasema hayo leo hapa mjini Tehran katika mazungumzo na Fayez Ghosn, Wa
ziri wa Ulinzi wa Lebanon.
Kuhusu matukio na harakati za ukombozi dhidi ya ubeberu katika eneo hili, Dakta Ahmadinejad amesisitiza kuwa zama za kupenda kujitanua za baadhi ya nchi duniani, zimefikia kikomo na kwamba ulimwengu sasa unakaribia kushuhudia mifumo ya kiadilifu na kibinadamu ikitawala duniani.
Fayez Ghosn Waziri wa Ulinzi wa Lebanon amepongeza uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Lebanon katika mapambano yake dhidi ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kueleza kuwa wananchi wa Lebanon hawawezi kusahau moyo wa upendo na misaada ya wananchi na serikali ya Iran katika vipindi vigumu na kwamba daima wananchi wa Lebanon watakuwa pamoja na wenzao wa Iran.
960765
captcha