IQNA

ISESCO kuanzisha mtandao wa Kiislamu wa utafiti

11:18 - March 15, 2012
Habari ID: 2292116
Shirika la Kiislamu, Elimu Sayansi na Utamaduni (ISESCO) litaandaa mkutano wa kwanza wa waratibu wa kitaifa kuhusu kuanzishwa mradi wa Mtandao wa Nchi za Kiislamu wa Utafiti na Elimu (PIREN) mnamo Machi 19-20 mwaka huu katika makao yake makuu huko Rabat, Morocco.
Kwa mujibu wa tovuti ya ISESCO, mtandao huo unalenga kuunganisha miundombinu ya teknolojia na mawasiliano katika nchi za Kiislamu, kuimarisha mawasiliano baina ya watafiti na maafisa wa elimu katika ulimwengu wa Kiislamu na kustawisha mabadilishano na mawasiliano baina yao kupitia PIREN na suhula zake.
Mkutano huo wa Rabat pia utatathmini hatua zilizopigwa katika ustawi wa Mitandao ya Kitaifa ya Utafiti na Elimu NREN huko Algeria, Misri, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kazakhstan, Malaysia, Morocco, Pakistan, Sudan, Turkey, Senegal na Nigeria.
ISESCO ni taasisi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC na ilianzishwa Mei mwaka 1979. ISESCO ndio taasisi kubwa zaidi ya Kiislamu katika uga wa kimataifa inayoshughulikia masuala ya elimu, sayansi na utamaduni.
972283
captcha