IQNA

Sayyid Nasrullah: Kuna njama za kutaka kuligawa eneo la Mashariki ya Kati

16:19 - March 17, 2012
Habari ID: 2292745
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, eneo la Mashariki ya Kati linakabiliwa na njama za kutaka kuligawa.
Sayyid Nasrullah ameelezea wasiwasi mkubwa alionao kuhusiana na Syria na kubainisha kwamba, utatuzi pekee wa mgogoro wa nchi hiyo ni njia za kisiasa na sio vinginevyo. Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amezitaka pande husika nchini Syria kuweka chini silaha na kukaa katika meza ya mazungumzo ya kisiasa.
Amesema Hizbullah inahofia Syria na Mashariki ya Kati kwa ujumla kutumbia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ameongeza kuwa, maandamano ya wananchi wa Syria na himaya yao kwa magezui yaliyofanywa na serikali ya Rais Bashar al Assad yanaonyesha kwamba, wananchi wa nchi hiyo hawataki vita wala uingiliaji wa kigeni katika masuala ya ndani ya nchi yao bali wanachotaka ni kupatiwa ufumbuzi mgogoro huo kwa njia za amani.
Kiongozi wa Hizbullah pia amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu mapinduzi ya wananchi wa Bahrain ambapo utawala wa Aal Khalifa unakandamiza kinyama maandamano ya amani.
Kuhusu hujuma ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza, Sayyid Nasrullah amewasifu wanamapambano wa Palestina kwa mshikamano wao wakati wa hujuma ya Wazayuni. Kiongozi wa Hizbullah amelaumu baadhi ya nchi za Kiarabu na vyombo vyao vya habari kwa kuwa pamoja na utawala haramu wa Israel na kulaumu harakati za mapambano Palestina kuwa eti ndizo zilizosababisha hujum ya Israel.

972841
captcha