Taarifa hiyo imewataka wananchi wa Bahrain kufanya jitihada kubwa zaidi za kumkomboa mwanaharakati Abdul Hadi al Khawaja anayeteseka katika jela za utawala wa Aal Khalifa.
Muungano wa 14 Februari umesisitiza kuwa dhulma ya watawala wa Bahrain imechoma na kuteketeza heshima na utukufu wa taifa hilo. Imesema kuwa maandamano yaliyofanywa na wanamapinduzi wa Bahrain Jumatano iliyopita chini ya kaulimbiu ya "Uhuru au Kufa Shahidi" yalikuwa awamu ya kwanza ya hasira za wananchi na kwamba awamu nyingine utafanyika katika siku zijazo kwa ajili ya kutangaza uungaji mkono kwa Abdul Hadi Al Khawaja.
Taarifa ya Muungano wa 14 Februari imemalizia kwa kusema kuwa iwapo al Khawaja atapatwa na madhara katika jela za utawala wa Aal Khalifa, taifa lote la Bahrain litachukua hatua kali za kutetea nembo hiyo kubwa ya kitaifa. 979363