Dr. Ali Mohyiddin Qurra Daghi, Naibu Mkurugenzi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu ametoa taarifa katika kongamano la Palestina huko Doha Qatar na kusema katika siku hii, Waislamu watafunga saumu kufungamana na wafungwa wa Palestina ambao wamepanga kususia chakula kama njia ya kulalamikia hali mbaya iliyoko katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel. Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu ina zaidi ya wanazuoni 60,000 wa Kishia na Kisuni duniani.
Harakati za Mapambano ya Palestina huko Ghaza pia zimesema saumu kama hivyo imeitishwa Jumatatu kama njia ya kutangaza mfungamano na wafungwa Wapalestina.
Katika taarifa, harakati hizo zimekosoa Mamlaka ya Ndani ya Palestina huko Ramallah inayoongozwa na Mahmoud Abbas kwa kuendelea kuwa na uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na kujaribu kuhuisha kile kinachotajwa kuwa ni mkono wa amani ambao ni pazia ya kuziba jinai za Wazayuni.
985849