Mahmoud Lotfiniya amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu kwa watoto ni muhimu kwa maisha yao na pia watoto wenye ulemavu wanapaswa kujumuishwa katika mafunzo hayo.
Amesema pamoja na kuwa kutoa mafunzo ya Qur'ani kwa watoto walemavu kuna changamoto kadhaa, kuna haja ya kubuni mbinu mwafaka za kuhakikisha wanapata mafunzo.
'Utafiti unaonyesha kuwa watoto wenye ulemavu wanaweza kuwashinda watoto wa kawaida katika nyanja mbalimbali za sayansi na ufundi na hata baadhi wamepata tuzo katika mashidano mbalimbali yakiwemo ya sayansi za Qur'ani,' amesema.
Amekumbusha kuwa idadi kubwa ya watu waliohifadhi Qur'ani katika nchi za Kiarabu ni watu wenye ulemavu wa macho na hivyo wanaweza kuwa kigezo.
990781