IQNA

Maulamaa wa Morocco walaani kuchomwa moto Qur'ani huko Marekani

20:14 - May 05, 2012
Habari ID: 2318883
Maulamaa wa Kiislamu wa Morocco wametoa taarifa wakilaani kitendo cha kasisi Terry Jones wa Marekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika jimbo la Florida.
Taarifa iliyotolewa na wanazuoni wa Kiislamu wa Morocco imesema kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu ni dhambi kubwa inayochochea hisia za Waislamu kote duniani.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa dhambi hiyo ni uhalifu mkubwa dhidi ya dini zote.
Wanazuoni hao wamesisitiza kuwa jinai hiyo imefanywa dhidi ya kitabu kinachohubiri kheri na amani na haiwezi kutetewa kwa njia yoyote ile.
Imesema vitendo kama hivyo haviwezi kuwalazimisha Waislamu kutupilia mbali thamani zao za kibinadamu na kwamba kitabu hicho kitaendelea kuhifadhiwa katika ntoyo za Waislamu kote duniani licha ya uhasama na vinyongo vya adui.
Taarifa hiyo imewataka wanafikra, watu wenye busara na waumini nchini Marekani na katika nchi nyingine duniani kushikamana kwa shabaha ya kupambana na aina zote za misimamo ya kupindukia mipaka katika masuala ya kidini. 999989
captcha