Kwa mujibu wa tovuti ya lacote, wizara hiyo imesisitiza kwamba maeneo hayo matakatifu ni sehemu ya turathi na utajiri wa kiutamaduni wa Tunisia na kulaani vikali hujuma dhidi ya maeneo hayo ya ibada. Huku akilaani vikali kitendo hicho Mahdi Mabrouk, Waziri wa Utamaduni wa Tunisia ametoa pendekezo la kubuniwa kamati maalumu itakayosimamia na kuchunga turathi na maeneo matakatifu kama hayo dhidi ya hujuma za watu waovu. Wakati huohuo, wizara yake imetangaza kwamba askari usalama wa nchi hiyo wanachunguza na kufuatilia watu waliohusika na hujuma hiyo. Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeashiria itikadi potofu za makundi ya Mawahabi kuhusiana na ziara katika maeneo matakatifu na kusema kuwa ndiyo yamekuwa yakiwachochea wafuasi wao kuharibu maeneo hayo.1008325