IQNA

Mahafali ya kimataifa ya kufarijika na Qur'ani yafanyika katika Haram ya Imam Hussein (as)

17:32 - July 03, 2012
Habari ID: 2360012
Mahafali ya kimataifa ya kufarijika na Qur'ani Tukufu imefanyika hivi karibuni katika Haram ya Imam Hussein (as).
Mahafali hiyo iliyoandaliwa na Darul Qur'an al-Karim inayofungamana na haram hiyo imewashirikisha makarii wa kimataifa kutoka nchi za Iran na Misri.
Mahafali hiyo ilifunguliwa kwa kiraa cha Usama Karbalai, mkuu wa Jumuiya ya Makarii na Mahafidh wa Darul Qur'ani al-Karim na kufuatiwa na kiraa ya Muhammad Mahmoud at-Tablawi, karii mashuhuri wa Misri na mkuu wa Jumuiya ya Makarii ya nchi hiyo.
Wageni wa Haram ya Imam Hussein (as) pia walihudhuria mahafali hiyo. Darul Qur'an al-Karim pia ina mipango ya kuandaa mahafali kama hiyo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo makarii mashuhuri wa Misri wamealikwa kushirki. 1043707
captcha