IQNA

Waziri Mkuu wa Iraq atembelea Haram ya Kadhimiya baada ya ushindi wa uchaguzi

12:44 - November 13, 2025
Habari ID: 3481509
IQNA – Waziri Mkuu wa Iraq, Muhammad Shia Al-Sudani, amesafiri hadi Kadhimiya, kaskazini mwa Baghdad, kutembelea makaburi matakatifu  baada ya kutangazwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iraq, Ofisi ya Habari ya Waziri Mkuu imetangaza kuwa Al-Sudani alielekea katika mji huo mtukufu baada ya muungano anaounga mkono kutangaza ushindi katika uchaguzi wa bunge.

Alitembelea makaburi matukufu ya Imam Hadi (AS) na Imam Hassan Askari (AS). Vyombo vya habari vya Iraq vimeripoti pia kuwa Al-Sudani alizuru maqbara ya Abu Hanifa Al-Nu’man katika mji wa Al-Adhamiyah.

Tume Kuu ya Uchaguzi ya Iraq ilitangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge Jumatano usiku.

Kulingana na matokeo hayo, Al-Sudani alibainisha kuwa muungano wake unaongoza kura na akatangaza utayari wa kuanza mashauriano ya kuunda serikali mpya.

“Muungano wa Ujenzi na Maendeleo uko nafasi ya kwanza na tutaanza mara moja mazungumzo ya kuunda serikali yenye ufanisi,” alisema katika tamko.

Aliongeza kuwa muungano wake unakaribisha makundi na mitazamo yote bila ubaguzi, kwa moyo wazi, na ameahidi kulinda maslahi ya Wairaq wote, wakiwemo wale ambao hawakushiriki katika uchaguzi.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa:

  • Muungano wa Ujenzi na Maendeleo uko nafasi ya kwanza kwa viti 46'
  •  Utawala wa Sheria nafasi ya pili kwa viti 3
  •  Harakati ya Al-Sadiqun nafasi ya tatu kwa viti 27
  •  Badr nafasi ya nne kwa viti 18

Matokeo haya yanaonyesha kuimarika kwa nafasi ya harakati za Kishia zilizo karibu na serikali kuu, na kuamua ushawishi wao katika bunge lijalo, hivyo kubadilisha mizani ya kisiasa ya ndani ya Iraq. Pia yanatoa fursa ya maamuzi yenye uratibu zaidi na kuimarisha nguvu ya serikali katika siasa za ndani na za kikanda.

4316581

captcha