IQNA

Muislamu Mjapani asema Qur'ani ni Kama “Dawa Iliyoponya Baada ya Madaktari Kushindwa”

17:33 - October 31, 2025
Habari ID: 3481442
IQNA – Mhubiri wa Kiislamu mzaliwa wa Japani, Fatima Atsuko Hoshino, amesema kuwa Qur'ani Tukufu imempa majibu ya maswali aliyokuwa nayo kwa muda mrefu na imemponya maradhi ambayo wataalamu wa tiba walishindwa kuyatibu.

Akizungumza katika kongamano lililopewa jina “Kutoka Atsuko hadi Fatima” lililoandaliwa na Idara ya Sayansi ya Qur'ani na Hadith katika Chuo Kikuu cha Isfahan, nchini Iran, Hoshino alielezea safari yake ya kiroho na athari ya Qur'ani Tukufu katika maisha yake.

Hoshino, ambaye alilelewa katika familia yenye mchanganyiko wa imani za Kibudha na Kishinto kabla ya kuingia Uislamu, alisema kuwa alipata ndani ya Qur'ani mwangaza na mwongozo aliokuwa akiuomba kwa muda mrefu.

"Nilitambua kuwa Qur'ani ina maelekezo kama vile dawa ya daktari," alisema. "Iliniponya na kuniepusha na maradhi ambayo madaktari na washauri walishindwa kuyatibu kwa miaka mingi."

Aliongeza kuwa Qur'ani ilimpa majibu ya maswali ya kuwepo ambayo yalikuwa yakimtatiza tangu ujana wake. Aliielezea kama mwongozo kamili unaotoa tiba si kwa mwili tu bali pia kwa roho.

Hoshino alifafanua kuwa kupitia kujifunza Uislamu, alikuja kuelewa maadili ambayo hakuwahi kukutana nayo katika tamaduni au imani alizokulia. "Kwa mara ya kwanza," alisema, "nilihisi furaha ya kusema ‘ndiyo’ kwa Mwenyezi Mungu na kwa wazazi wangu. Nilielewa kuwa utu, imani, na kiroho ni mambo yanayoweza kukua kila siku kwa juhudi, ilhali mwili, ambao awali ndio ulikuwa kitovu cha fikra zangu , unaelekea kudhoofika."

Aliifananisha mitihani aliyopitia baada ya kuingia Uislamu na hali ya kuwa ndani ya sufuria aina ya pressure cooker. "Giza na mashinikizo niliyopitia vilinikumbusha hali hiyo," alisema. "Mwenyezi Mungu anataka nipikwe na kuwa mwema mapema."

Licha ya changamoto hizo, Hoshino alisema kuwa alipata uhuru wa kweli kupitia kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu. "Bado napenda uhuru," alisisitiza, "lakini sasa nimeupata katika ibada kwa Mungu. Nimeelewa kuwa uhuru wa kweli upo Akhera, na njia ya kuelekea huko ndiyo ninayoitembea sasa."

Hoshino, ambaye huzungumza mara kwa mara katika mikutano ya kidini na kielimu nchini Iran, anajulikana kwa tafakuri zake kuhusu imani, kiroho, na nafasi ya mwanamke katika Uislamu , mada zinazovutia hadhira ya

3495213

captcha