
Gazeti hilo la kila siku liliripoti hivi karibuni kuwa Waziri wa Vita wa Marekani amewafuta kazi au kuwazuia kupandishwa vyeo zaidi ya majenerali na makamanda 20 katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, bila maelezo ya wazi.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa baadhi ya maafisa hao waliondolewa kwa sababu ya kutoa maoni yao au kupinga maamuzi ya kisiasa, yakiwemo mashambulizi katika eneo la Karibiani na kutokubaliana kwao kuhusu Iran.
Katika kujibu ripoti hiyo, msemaji wa Iran alinukuu aya ya 14 ya Surah Al-Hashr katika Qur’ani Tukufu isemayo: “Unadhani kuwa wao ni wamoja, lakini nyoyo zao zimegawanyika.”
Kwa mujibu wa New York Times, Waziri wa Vita wa Marekani, Pete Hegseth, amewafuta kazi au kuwaweka pembeni angalau majenerali na makamanda 24, hatua inayobadilisha kabisa uongozi wa kijeshi wa Marekani.
Hatua hizo, ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika miongo ya karibuni, zimezua taharuki miongoni mwa maafisa waandamizi wa jeshi na kuibua hali ya kutoaminiana, hali inayowalazimu kuchukua misimamo tofauti katikati ya mabadiliko yasiyo ya kawaida ya uongozi.
Seneta Elissa Slotkin ametaja hatua hizo za Hegseth kuhusu rasilimali watu kama “msako wa kisiasa,” akieleza wasiwasi wake kuhusu kupotea kwa viongozi wenye uzoefu ndani ya jeshi la Marekani.
3495356