IQNA

Libya yaandaa Mashindano ya Qur’ani kwa wanafunzi

12:47 - November 13, 2025
Habari ID: 3481510
IQNA – Mashindano ya kuhifadhi Qur’ani kwa wanafunzi wa shule yameanza mjini Zliten, Libya, Jumanne, tarehe 11 Novemba.

Mashindano hayo yameandaliwa chini ya usimamizi wa Idara ya Shughuli za Shule ya Wizara ya Elimu ya Libya katika mji wa Zliten.

Kauli mbiu ya mashindano haya ni: “Kitabu cha Mwenyezi Mungu Kinatuunganisha”, na yamepangwa kwa mujibu wa mpango maalum wa shughuli za shule kwa mwaka wa masomo 2025-2026.

Kwa mujibu wa tovuti ya Ain Libya, jumla ya wanafunzi 60 wamehudhuria mashindano hayo. Washiriki 40 walishindana katika uwanja wa kuhifadhi Qur’ani. Washiriki 20 walishindana katika kipengele cha kutoa khutba

Malengo ya mashindano haya ni kuimarisha thamani za Qur’ani miongoni mwa kizazi kipya na kuendeleza roho ya ushindani katika kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.

Libya imekuwa miongoni mwa nchi zenye shughuli nyingi katika kuandaa mashindano ya Qur’ani ya kitaifa na kimataifa. Mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Libya toleo la 13 yalifanyika mwishoni mwa Septemba mwaka huu, yakihusisha washiriki 120 kutoka zaidi ya nchi 70.

3495373

captcha