IQNA

Wanafunzi Waislamu Marekani wataka uchunguzi baada ya Qur'ani Tukufu kuvunjiwa heshima

16:00 - November 05, 2025
Habari ID: 3481472
IQNA – Chuo Kikuu cha Houston kilichopo jimbo la Texas, Marekani, kimetangaza kuwa kinachunguza tukio la kuvunjia heshima nakala ya Qur'an Tukufu wakati wa mkusanyiko wa wanafunzi Waislamu.

Wanafunzi Waislamu katika chuo hicho wanataka hatua zichukuliwe baada ya shambulio la chuki dhidi ya Uislamu lililotokea katika hafla ya chuoni na kuacha jamii ya Waislamu ikiwa na mshtuko mkubwa.

Kwa mujibu wa Jumuiya ya Wanafunzi Waislamu ya UH (UH MSA), tukio hilo lilitokea Alhamisi, Oktoba 30, katika bustani ya Lynn Eusan. Mtu mmoja anaripotiwa kuingia katika eneo walilokuwa wametenga kwa ajili ya ibada, akapaza sauti kupitia kipaza sauti akitoa ujumbe wa chuki dhidi ya Uislamu, kisha akatupa nakala ya Qur'ani ndani ya moto wa wazi.

Kufuatia tukio hilo, UH MSA inaitaka chuo kutoa tamko rasmi la kuonyesha dhamira yake ya kuwalinda wanafunzi Waislamu, kuwapatia eneo salama la kukusanyika, na kuweka zuio la kurudi chuoni kwa mtu huyo.

Katika tamko kwa gazeti la Chron, uongozi wa chuo umesema: "Chuo Kikuu cha Houston kinachukulia kwa uzito madai yote ya kuvunjiwa heshima wanajamii wetu. Polisi wa Chuo (UHPD) wamejulishwa na wanachunguza tukio hili."

3495261

Habari zinazohusiana
captcha