IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’an kwa Wanafunzi Waislamu: Viongozi na Kamati Tendaji Wateuliwa

19:33 - November 14, 2025
Habari ID: 3481513
IQNA – Mwenyekiti, katibu na wajumbe wa kamati tendaji ya Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur’an kwa Wanafunzi Waislamu wametambulishwa rasmi.

Ali Montazeri, Mkuu wa Akademia ya Kielimu, Kitamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR), aliwateua viongozi hao kwa waraka maalum siku ya Jumanne.

Kwa mujibu wa ofisi ya mahusiano ya umma ya ACECR, Montazeri alimteua Mahmoud Aligou, Naibu wa Kitengo cha Utamaduni wa kituo hicho, kuwa Mwenyekiti, na Jalil Bayt Mashali, Mkuu wa Shirika la Qur’an la Wanazuoni wa Iran, kuwa Katibu wa toleo hili la mashindano ya kimataifa ya Qur’an.

Aidha, Mohsen Masjeedjamei, Laleh Shakour Shahabi na Masoumeh Sabour wameteuliwa kuwa wajumbe wa kamati tendaji ya toleo la saba.

Montazeri alisema katika waraka wake: “Tunatarajia kwa ushirikiano wa wajumbe watukufu wa kamati tendaji na kwa kutegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, mazingira yatandaliwa kwa ajili ya kufanikisha kwa heshima toleo hili la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’an kwa Wanafunzi Waislamu, na nyinyi mtapata ufanisi katika kutekeleza majukumu yenu.”

Shirika la Qur’an la Wanazuoni wa Iran, linalohusiana na ACECR, limekuwa likiandaa mashindano haya tangu mwaka 2006 kwa lengo la kukuza mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi wa ulimwengu wa Kiislamu na kuinua kiwango cha shughuli za Qur’an.

Mashindano ya mwaka huu yanakuja baada ya mafanikio ya matoleo sita yaliyopita, ambayo yalihusisha washiriki kutoka zaidi ya nchi 85 na kuleta athari kubwa katika ushiriki wa Qur’an na utamaduni kote ulimwengu wa Kiislamu.

Toleo la sita lilifanyika katika mji mtukufu wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran, mwezi Aprili 2018.

4316193

Habari zinazohusiana
captcha