IQNA

Sala ya kuomba mvua taifa zima yaswaliwa Saudia

12:39 - November 13, 2025
Habari ID: 3481508
IQNA – Sala ya Istisqa (swala ya kuomba mvua) imeswaliwa leo Alhamisi, kufuatia sunnah ya Mtume Muhammad (SAW) ya kuomba rehema ya Mwenyezi Mungu kupitia ibada ya pamoja. Swala hiyo imeswaliwa kufuatia ombi la Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudi (SPA), agizo la kifalme liliwahimiza watu kote nchini kushiriki katika swala hiyo kama njia ya kuomba mvua na rehema ya Mwenyezi Mungu wakati wa ukame.

Baada ya amri hiyo ya kifalme, Sheikh Saleh Al-Fawzan, mwanazuoni mashuhuri na Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni Wakuu, ambaye pia ni mkuu wa Idara Kuu ya Utafiti wa Kielimu na Fatwa, awali aliwataka watu kuhudhuria Swala ya Istisqa siku ya leo Alhamisi, tarehe 13 Novemba.

“Swala ya Istisqa ni miongoni mwa sunnah zilizothibitishwa za Mtume Muhammad (SAW). Wakati Madina ilipokumbwa na ukame, Mtume alikwenda uwanjani, akaongoza watu katika rakaa mbili, akatoa khutba na kumuomba Mwenyezi Mungu awateremshie mvua,” alisema Sheikh Al-Fawzan.

Akaongeza: “Kwa kufuata sunnah hii tukufu, khatibu anapaswa kuomba kwa unyenyekevu na kumlilia Mwenyezi Mungu awateremshie mvua, huku akihimiza watu kutubu, kufanya matendo mema kama swala, funga na kutoa sadaka, na kuacha chuki na uadui ili dua zao zikubaliwe.”

Kwa mujibu wa agizo la kifalme, Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Da’wa na Mwongozo  swala hiyo iliswaliwa katika misikiti yote ya Saudi Arabia dakika 15 baada ya kuchomoza kwa jua siku ya Alhamisi.

Wizara awali ilielekeza ofisi zake za mikoa kuhakikisha maandalizi yote yamekamilika katika misikiti na viwanja vilivyoteuliwa, ikiwemo Makka, Madina na Riyadh, ili kuwapokea waumini na kuweka mazingira muafaka kwa ibada hiyo ya pamoja.

3495367

Habari zinazohusiana
captcha