IQNA

Malaysia Yatumia Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) Kuharakisha Uchapishaji Nakala za Qur'ani

17:22 - October 31, 2025
Habari ID: 3481441
IQNA – Serikali ya Malaysia imezindua mfumo mpya uitwao iTAQ unaotumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kuharakisha mchakato wa kuthibitisha usahihi wa machapisho ya nakala za Qur'ani Tukufu.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Malaysia (KDN) siku ya Jumatano ilizindua rasmi mfumo wa Intelligence Tashih Al-Quran (iTAQ), unaolenga kuimarisha kasi na ufanisi wa ukaguzi wa maandiko ya Qur'ani yanayochapishwa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsul Anuar Nasarah, alisema kuwa mfumo huo unaoongozwa na Lembaga Pengawalan dan Pelesenan Pencetakan Al-Quran (LPPPQ) utaimarisha juhudi za kulinda usahidi nakala Qur'ani Tukufu kwa kuzingatia changamoto za kisasa zinazozidi kuwa ngumu.

Alisisitiza kuwa licha ya kuanzisha ubunifu kama mfumo wa iTAQ, LPPPQ haijapuuza jukumu lake la kuhakikisha usahihi wa maandiko ya Qur'ani Tukufu na ulinganifu wake na sheria za Kiislamu.

"Bodi hii ina jukumu la kulinda utukufu wa Qur'ani. Si kizuizi cha maendeleo, bali ni chujio dhidi ya madhara yanayoweza kuathiri usomaji sahihi na uelewa wa Qur'ani miongoni mwa Waislamu," alisema katika mkutano wa Multaqa MADANI uliofanyika Sepang pamoja na kamati za LPPPQ.

Mbali na mfumo wa iTAQ, wizara hiyo pia ilizindua Moduli ya Utaalamu kwa Wajumbe wa Ukaguzi wa Qur'ani (ProQuran), inayolenga kuinua ubora wa washauri wa Qur'ani wanaoteuliwa na sekta ya uchapishaji.

3495205

Habari zinazohusiana
captcha