IQNA

Mwaliko wa mashindano ya Qur'ani kwa wanafunzi wa zamani wa al-Azhar

12:59 - July 04, 2012
Habari ID: 2360867
Jumuiya ya Kimataifa ya Wanafunzi Waliohitimu Masomo yao Al-Azhar nchini Misri imetoa mwaliko kwa wanafunzi wa kigeni waliohitimu masomo yao katika chuo hicho cha kidini kuandikisha majina yao hadi kufikia tarehe 15 Julai kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya Qur'ani Tukufu yanayotazamiwa kufanyika hivi karibuni nchini humo.
Mashindano hayo yatakuwa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani. Kwa mujibu wa tovuti ya al-Azhar wanafunzi wote wa zamani wa chuo hicho cha kidini wanaweza kushiriki kwenye mashindano hayo.
Akifafanua suala hilo, Usama Yasin, mkuu wa halmashauri ya idara ya jumuiya iliyotajwa amesema lengo kuu la kufanyika mashindano hayo ni kuimarisha thamani za kiutu na vilevile kuhimiza mashindano salama ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu miongoni mwa wanafunzi wa al-Azhar. Amesema mashindano hayo yatafanyika katika makundi mawili ya hifdhi na kiraa, ambapo washiriki wa kundi la hifdhi watagawanywa katika makundi manne ya hifdhi ya Qur'ani nzima, robo tatu, nusu na robo moja ya Qur'ani Tukufu.
Yasin ameendelea kusema washindi wa kwanza 10 katika kundi la hifdhi ya Qur'ani nzima watazawadiwa juneih 1000 kila mmoja, 10 wa kundi la pili juneih 750, 10 wa kundi la tatu juneih 500 na 10 wa kundi la mwisho juneih 250.
Ameongeza kuwa washindi 5 katika kundi la kiraa na tajwidi watatunukiwa juneih 250 kila mmoja. Tarehe hasa ya kufanyika mashindano hayo bado haijatangazwa na wahusika. 1044097
captcha