Kwa mujibu wa tovuti ya Safirnews, mashindano hayo ya kiraa ya Qur'ani Tukufu ambayo yatafanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani yatawahusisha vijana wa miaka 8 hadi 26.
Duru za utangulizi za mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika tarehe 12, 13 na 14 za mwezi huu wa Julai kabla ya washindi kushiriki katika mashindano ya mwisho yaliyopangwa kufanyika tarehe 17 Agosti.
Watu walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo wana fursa ya hadi kufikia tarehe 10 Julai kusajili majina yao kupitia mtandao wa intaneti. Washindi wa mashindano hayo watatunukiwa zawadi nono ikiwemo ya kuhiji mjini Makka Saudi Arabia. 1044766