Akizungumza katika sherehe za kuwaenzi mahafidh hao, Abdulswamad Pat, mwanazuoni wa mji huo amesema kwamba kuandaliwa kwa sherehe kama hizo ni fahari kubwa kwa wakazi wa mji huo na kwamba kupewa malezi vijana kama hao ni chanzo cha kubarikiwa Waislamu humu duniani na huko Akhera.
Muhammad Gauhar mwanazuoni mwingine aliyezungumza katika sherehe hizo ameashiria suala la kudumu milele thamani za Qur'ani kwa jamii ya mwanadamu na kusema kuwa baraka na neema za Mwenyezi Mungu huteremka katika kila sehemu ambayo kitabu hicho cha mbinguni huwa kinasomwa.
Mahafidh watano bora wa Uturuki walienziwa katika shehere hizo ambapo pia walipewa nafasi ya kuwafariji hadhirina kwa visomo vyao vya kuvutia vya Qur'ani Tukufu. 1044482