IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaanza Malaysia

16:59 - July 07, 2012
Habari ID: 2362657
Sherehe za ufunguzi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu zilifanyika hapo jana usiku katika Kituo cha Kibiashara ya Kimataifa cha Malaysia mjini Kuala Lumpur.
Amin Pouya, mshindi wa pili katika kundi la kiraa katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika mwaka jana nchini Iran amechaguliwa kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo na anatazamiwa kupewa fursa ya kusoma katika mashindano hayo ya Malaysia hapo kesho Jumapili usiku. Msomaji huyo wa Qur'ani wa Iran ana nafasi nzuri ya kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano hayo.
Mashidano hayo ambayo yanahesabiwa kuwa mashindano makongwe zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu yanawashirikisha washindani 60 kutoka nchi 42 za dunia. Yamedhaminiwa na Taasisi ya Ustawi wa Kiislamu ya Malaysia chini ya anwani ya 'Qur'ani Tukufu; Hutayarisha Uwanja wa Utukufu wa Umma wa Kiislamu ulio na Misimamo ya Wastani.'
Mashindano hayo yatamalizika tarehe 13 Julai ambapo washindi watatunukiwa zawadi. 1046366
captcha