IQNA

Mafunzo ya Qur'ani kutolewa Pakistan

17:14 - July 07, 2012
Habari ID: 2362660
Mafunzo ya kiraa na hifdhi ya Qur'ani Tukufu kwa wanachuo wa Kishia nchini Pakistan yamepangwa kuanza kutolewa siku ya Jumapili Julai 22 hadi Ujumaa tarehe 10 Agosti katika mji wa Jalalpur ilioko katika jimbo la Punjab.
Mbali na mafunzo hayo, wataalamu na wanazuoni wa masuala ya kidini watazungumzia masuala mbalimbali ya Kiislamu na Qur'ani.
Mafunzo hayo huandaliwa kila mwaka na Hujjatul Islam wal Muslimeen Muntadhar Mahdi, mwanafunzi wa Jamiutul Mustafa (saw) al-Alamiya ambaye pia ni mwanazuoni mashuhuri katika mji wa Jalalpur.
Walio na hamu ya kushiriki mafunzo hayo wamealikwa kusajili majina yao kabla ya Julai 22. 1044477
captcha