Gazeti la al Iqtisadiyya linalochapishwa nchini Saudi Arabia liomeripoti kuwa ratiba hizo zilijumuisha semina ya masuala ya kitaalamu kwa kushirikiana na vyuo vikuu na taasisi za utafiti na jumuiya za Kiislamu barani Afrika.
Sheikh Abdullah bin Abdul Aziz al Muslih ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani na Suna za Mtume (saw) amesema kuwa ratiba hizo zilijumuisha uhuishaji wa mwenendo wa uchapishaji na usambzaji wa vitabu na tarjumi zinazohusiana na masuala ya muujiza wa kisayansi wa Qur'ani Tukufu ambazo zimefanyika katika nchi kama Tanzania na Kenya.
Ratiba hizo zilihudhuriwa na ujumbe wa wanachama wa Kamati ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani katika taasisi za Kiislamu na misikiti ya nchi za Kiafrika.
Ujumbe huo pia ulitoa zawadi ya vitabu vya Kiislamu vinavyohusu muujiza wa kisayansi wa Qur'ani Tukufu kwa maktaba za Chuo Kikuu cha Kiislamu mji mjini Morogoro Tanzania. 1047620