IQNA

Sherehe za kuwaenzi mahafidh wa Qur'ani zafanyika Uturuki

13:00 - July 09, 2012
Habari ID: 2364202
Sherehe za kushukuru na kuwaenzi mahafidh wa Qur'ani Tukufu zimefanyika katika msikiti wa Ijumaa wa mji wa Tortum ulioko katika mkoa wa Erzurum nchini Uturuki.
Wanazuoni na wataalamu wa masuala ya Qur'ani walihudhuria sherehe hizo ambazo zilianza kwa kisomo cha Qur'ani. Waliozungumza kwenye sherehe hizo walizungumzia umuhimu wa kusoma na kujifunza hifdhi ya Qur'ani.
Sherehe hizo zimefanyika kwa lengo la kuwaenzi wanafunzi 18 waliofanikiwa kuhifadhi kitabu hicho cha mbinguni kati ya wanafunzi wote 60 wa mji huo waliokuwa wakijishughulisha na suala hilo.
Akisisitiza juu ya umuhimu wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu, Mustafa Aghirman, muhadhiri katika Chuo Kikuu cha Ataturk amesema si rahisi kwa kila mtu kufukia heshima na utukufu wa kuhifadhi Qur'ani na kwamba Mtume Mtukufu alikuwa akisisitiza sana juu ya umuhimu wa hifdhi ya kitabu hicho kitakatifu.
Waliofanikiwa kuhifadhi Qur'ani walienziwa na kutunukiwa zawadi katika sherehe hizo zilizofanyika siku ya Jumamosi. 1048244
captcha