IQNA

Maqarii wa Misri kushiriki vikao vya Qur’ani Mwezi wa Ramadhani

16:47 - July 10, 2012
Habari ID: 2365077
Shirika la Wakfu katika mkoa wa Kermanshah nchini Iran limeandaa vikao kadhaa vya Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambavyo vitawashirikisha maqarii wa Qur’ani kutoka Misri.
Hayo yametangazwa na Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika Shirika la Wakfu mkoani Kermanshah Sheikh Mohsen Suleimani ambaye ameongeza kuwa vikao hivyo vya Qur’ani vitafanyika katika misikiti na maeneo matakatifu mkoani humo.
‘Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa nzuri kwa wale wanaotaka kujikurubisha zaidi na Qur’ani Tukufu,’ ameongeza.
Katika upande mwingine maqarii wa Iran wameelekea katika nchi mbalimbali duniani kushiriki katika vikao vya Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
1048781
captcha