IQNA

Washiriki mashindano ya Qur’ani Dubai waanza kujiandikisha

17:36 - July 10, 2012
Habari ID: 2365437
Washiriki katika mashindano ya hifdhi ya Qur’ani Tukufu makhsusi kwa ajili ya wasichana huko Dubai wameanza kujiandikisha leo Jumanne.
Kituo cha habari cha Khaleej Time kimeripoti kuwa mashindano hayo ni sehemu ya ratiba ya Kongamano la Sita la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani linalosimamiwa na Jumuiya ya Shughuli za Kibinadamu na Masuala ya Kiislamu ya Dubai.
Mashindano ya mwaka huu yatafanyika kwa jina la “Mahala Iliposhuka Qur’ani”.
Wasichana watakaoshiriki katika mashindano hayo watachuana katika vitengo vya hifdhi ya Qur’ani nzima, hifdhi ya juzuu 20, juzuu 10, na juzuu 5.
Tarehe rasmi ya kufanyika mashindano hayo itatangazwa baada ya kuandisha majina ya washiriki.
Miongoni mwa malengo ya mashindano hayo ni kuzidisha na kustawisha maarifa ya kidini katika matabaka mbalimbali ya jamii na kuwaunganisha na Qur’ani Tukufu kupitia njia ya kuwahamasisha kuhifadhi Qur’ani na kuielewa. 1049750
captcha