IQNA

Uchunguzi wa Pew:

Mataifa mengi ya Mashariki ya Kati yanataka sheria za Qur’ani

15:21 - July 11, 2012
Habari ID: 2366335
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Pew ya Marekani umebaini kuwa licha ya kupita mwaka mmoja sasa tangu baada ya kuanza mwamko wa Kiislamu, harakati za demokrasia bado inapendwa na kukubaliwa na watu wengi katika nchi sita za Waislamu zilizokumbwa na mapinduzi ya wananchi na kwanba watu wengi katika nchi hizo wanataka sheria zinazotokana na mafundisho ya Qur’ani.
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanasema kuwa asilimia 67 ya watu wa Misri na asilimia 63 ya Watunusia, nchi mbili ambazo zilikuwa za kwanza kuzing’atua madaraklani tawala za kidikteta, wanaamini kuwa mifumo inayotawala sasa katika nchi zao ni bora zaidi ya tawala ziliong’olewa madarakani.
Ripoti ya Pew imesema kuwa asilimia 45 ya Watunisia wanaamini kuwa nchi hiyo imekuwa na hali bora zaidi baada ya kuondolewa madarakani dikteta Bin Ali. Ripoti ya Pew inasisitiza kuwa Uislamu una nafasi muhimu katika nchi zote za Mashariki ya Kati isipokuwa Lebanon ambako kuna idadi kubwa ya Wakristo ambao ni kundi la waliowachache nchini humo.
Nchini Pakistan asilimia 82 wanataka sheria za nchi hiyo zioane kikamilifu na Qur’ani. Asilimia 72 ya Wajordan, asilimia 60 ya Wamisri, asilimia 23 ya Watunisia na asilimia 17 ya watu wa Uturuki na Lebanon pia wanaafikiana na suala hilo.
Uchunguzi wa maoni wa taasisi ya Pew umefanyika katika miezi ya Machi na Aprili mwaka huu na umehusisha watu elfu moja katika kila nchi ya Waislamu. 1050466
captcha