Ripota wa IQNA kusini magharibi mwa Asia amesema kuwa taasisi hiyo Ijumaa Ijumaa ijayo imepanga kuitisha kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuelimisha na kutoa mafunzo ya sayansi ya Qur’ani Tukufu.
Maulamaa na wanafikra wakubwa wa Kiislamu wa India watachunguza mafundisho ya neno la Mungu, masuala na matatizo ya Kiislamu na kuwaelimisha hadhirina maana ya aya za kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.
Ratiba nyingine zitakazofanyika katika kongamano hilo ni pamoja na mashindano ya Qur’ani, semina na vikao vitakavyusu elimu na maarifa ya Qur’ani. 1051197