Kituo cha upashaji habari cha “Ic-el” kimeripoti kuwa, watu wote wanaruhusiwa kushiriki kwenye mashindano hayo yatakayofanyika katika siku za tarehe 23 hadi 25 za mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Kituo cha Kiislamu mjini London.
Kituo hicho pia kitakuwa mwenyeji wa mashindano mengine ya hifdhi ya Qur’ani makhsusi kwa watoto wadogo yatakayofanyika tarehe 14 Ramadhani.
Ratiba nyingine iliyopangwa kufanyika katika mwezi wa Ramadhani ni masomo ya Qur’ani. Ratiba hiyo itajumuisha vikao vya mihadhara ya kidini itakayotolewa kila siku saa moja kabla ya swala ya Magharibi.
Vilevile kutatolewa masomo ya Qur’ani kwa wanawake na vijana. 1052149