Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Elimu ya Jumuiya za Kidini nchini Uturuki Ali Arbash amesema mji wa Düzce ni makazi ya mahafidh wa Qur'ani Tukufu na kwamba wakazi wengi wa mji huo wamepata fahari ya kuhifadhi kitabu chote cha Mwenyezi Mungu. Ameongeza kuwa Niyazi Ozcelik ni miongoni mwa wakazi wa mji wa Düzce ambaye ameweza kuhifadhi kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu akiwa na umri wa miaka 86 na anaweza kuwa kigezo bora cha wale wanaotaka kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Msomi na mwanafikra wa Kiislamu wa Uturuki Selami Emen aliyehudhuria sherehe hizo amesema kuwa watu waliofanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima wakiwa na umri wa miaka 86 ni wachache mno na kwamba suala hilo ni fahari kubwa kwa kila Muislamu.
Niyazi Ozcelik amesema katika sherehe hizo kwamba anamshukuru Allah kwa kumpa taufiki ya kuhifadhi Qur'ani nzima na kusema kuwa hiyo ni saada na ufanisi mkubwa kwake yeye. 1052596