Duru hiyo itafanyika katika fremu ya mpango wa 11 wa Ramadhani wa Idara ya Utalii na Masoko ya Dubai chini ya kaulimbiu ya "Upepo wa Rehma".
Masomo hayo ya hifdhi na kutadabari ndani ya aya za Qur'ani yataendelea kwa kipindi cha siku tatu na washiriki watafundishwa njia za hifdhi ya Qur'ani na jinsi ya kutadabari na kutafakari katika aya za kitabu hicho.
Duru ya kwanza ya masomo hayo ya hifdhi ya Qur'ani ilifanyika Alkhamisi hadi Jumamosi ya jana ikiwashirikisha wanawake 26 na wanaume 13. Mhadhiri msaidi wa Chuo Kikuu cha al Qasim cha Saudi Arabia Ibrahim bin Abdullah al Duwaish ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya malezi na familia alihutubia vikao vya masomo hayo. 1052979