Mashindano hayo yatasimamiwa na Msikiti wa al Rawdah katika vitengo vinne vya watu wenye umri wa chini ya miaka 7, miaka 8-11, 12-15, na 16-25.
Watoto wenye umri wa chini ya miaka 7 watashindana kuhifadhi sura za Jinn na Naziat, umri wa miaka 8-11 sura za Hadid na Qamar, umri wa miaka 12-15 Raad na Ibrahim na wale wenye umri wa miaka 16-25 watashindana kuhifadhi Suratun Nisaa.
Mwishoni mwa mashindano hayo washindi 3 bora wa kila kundi watatunukiwa zawadi kutoka Msikiti wa Al Rawdah.
Sambamba na mashindano hayo kutafanyika mashindano mengine ya kiutamaduni yaliyopewa jina la "Mwezi Ramadhani" ambayo yatahusu maswali na majibu. 1052942