Imearifiwa kwa polisi wametumia marungu na gesi ya kutoa machozi kuwatawanya Waislamu waliokuwa wakibainisha malalamiko yao dhidi ya serikali ndani ya msikiti huo.
Msemaji wa serikali ya Ethiopia Shimeles Kemal amedai kuwa Waislamu wanatumia misikiti kwa malengo ya kisiasa. Waislamu wameendeleza maandamano ya kutaka waachiliwe huru wenzao waliotiwa nguvuni.
Waislamu Ethiopia wanailaumu serikali kwa kutaka kuwapandikizia viongozi vibaraka. Aidha serikali ya Ethiopia imelaumiwa kwa kutaka kuwalazimisha Waislamu Ethiopia kufuata pote lijulikanalo kama Ahbash.
Waislamu wanatabiriwa kuwa takribani nusu ya watu wote milioni 94 nchini Ethiopia. Chama cha upinzani cha ENTC kimelaani vyombo vya habari vya kimataifa kwa kunyamazia kimya jinai za serikali ya Ethiopia dhidi ya Waislamu nchini humo.
1053264